×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

image

Habari za UN, Jifunze Kiswahili: Uchambuzi wa neno, "RUWI" | | Habari za UN

Jifunze Kiswahili: Uchambuzi wa neno, "RUWI" | | Habari za UN

Sasa ni wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili. Leo tunafafanuliwa maana ya neno "RUWI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.

Kuna baadhi ya watu ambao wana uwezo wa kufanya udanganyifu bila ya kuhofia kitu chochote kile. Hawa ni watu wanaweza kuwa wanafanya ulaghai, bila hofu yoyote. Na ulaghai unaweza kuwa ni wa mara kwa mara. Mwongo, anaweza kuwa mzushi, anaweza kuwa mzandiki, tapeli, bazazi na kadhalika. Mtu wa namna hii kwa Uswahili anaitwa ruwi. Ruwi ni mtu mwenye tabia ya kufanya udanganyifu bila ya kuhofia kitu chochote. Yaani, hana woga wa namna yoyote katika kufanya kwake udanganyifu, kufanya kwake uwongo, uzandiki, uzushi, utapeli na ubazazi.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE