×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

Habari za UN, Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni… – Texto para ler

Habari za UN, Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama" | | Habari za UN

Intermediário 2 lição de Suaíli para praticar a leitura

Comece a aprender esta lição agora

Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama" | | Habari za UN

Na sasa kama nilivyokuahidi, ni wasaa wa kujifunza Kiswahili na leo hii nampisha Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) nchini Tanzania. Si mwingine bali ni Dkt. Mwanahija Ally Juma akituchambulia methali: Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama!

Mama ni mama hata kama ni rikwama. Mama ni mzazi mwanamke ambaye mara nyingi anachukua nafasi kubwa katika kumleta au kumzaa mtoto. Na anachukua nafasi kubwa katika kumhudumia mtoto tokea yuko tumboni hadi anazaliwa, hadi kukua kwake.

Na rikwama ni kifaa ambacho kinatumika kubebea mizigo. Kwa hiyo, hata kama mama anafanya kazi nyingi, ana nafasi kubwa katika malezi, ana shughuli nyingi za kumhudumikia mtoto, anabeba mazuri na mabaya, shida na dhiki, lakini bado atakuwa ni mama, na ana umuhimu sana katika familia na katika jamii. Kwa hiyo, mama ni mama hata kama ni rikwama.

Hata kama mama analazimika kufanya pilka nyingi, kubeba machungu, kubeba maovu, kubeba furaha, kubeba dhiki, kubeba shida, lakini bado ni mama na anastahili kutunzwa. Anastahili kupewa heshima. Kufikiriwa kwa mujibu wa uzito wake. Kwa kuwa ni rikwama anachukuliwa kama ni kitu ambacho kimetelekezwa kubeba vitu vizuri, vitu vichafu mbalimbali. Kazi yake ni kuzibeba tu lakini thamani yake ni ndogo. Ikimaliza kubeba inawekwa pembeni. Kwa hiyo mama ni mama. Bado anayo nafasi ya kuthaminiwa, ya kusaidiwa. Anayo nafasi ya kupewa umuhimu na uzito unaofaa hata kama ana shida nyingi ambazo zinamsibu na anajitwika na mazonge mengi kutokea uzazi, malezi, shida, matatizo, dhiki za watoto, na dhiki zake yeye bado zinamkabidhi. Lakini bado ni mama na anastahili heshima yote.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE