Jifunze kiswahili: Je, wajua maana ya neno "KUYEYESA"? | | Habari za UN
Na sasa ni wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili. Leo tunafafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA". Na mtaalam wetu Onni Sigalla. Huyu ni Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.
Mara nyingi tunafanya usaidizi kwa wenzetu na hasa ambao wamepatwa na maradhi kwa muda mrefu, wameishiwa nguvu au kwa mtu ambaye umri wake umemsogea sana na anahitaji usaidizi. Kitendo hicho si usaidizi kama ambavyo tunasema ila tunaweza tukasema ni uyeyesaji. Yaani, unayeyesa, au unayeyeswa, au unayeyesesha mtu ambaye aghalabu; ni mgonjwa ili aweze kutembea au kukua na nguvu tena ili aweze kutembea. Kwa hiyo, mtu unapomsaidia, mtu aweze kutembea, aweze kujongea mahali fulani, basi unakuwa unamyeyesa na kama ni wewe mwenyewe basi unayeyesewa na kadhalika.