Ibrahim ana mchumba mpya.
Jina la mchumba wake ni Rebeca.
Ibrahim anataka kumuandalia Rebeca chakula cha usiku.
Anaenda katika duka la vyakula.
Ibrahim anachukua kikapu na mkokoteni.
Anatembea kupita safu ya mboga za majani.
Anaangalia samaki ndani ya friji.
Anasimama karibu na dirisha la saladi.
Mwisho, anaondoka dukani humo.
Ibrahim anaenda nyumbani na kuagiza piza.
Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na Ibrahim.
Nina mchumba mpya.
Jina lake ni Rebeca.
Ninataka kuandaa chakula cha jioni kwa ajili ya Rebeca.
Ninaenda katika duka la vyakula.
Ninachukua kikapu na mkokoteni.
Ninatembea kupita safu ya mboga za majani.
Ninaangalia samaki ndani ya friji.
Ninasimama karibu na dirisha la saladi.
Mwisho, nikaondoka dukani humo.
Nikaenda nyumbani na kuagiza piza.
Maswali.
1) Ibrahim ana mchumba mpya anaeitwa Rebeca. Je, Ibrahim ana mchumba mpya? Ndiyo, Ibrahim ana mchumba mpya. Jina lake ni Rebeca.
2) Ibrahim anataka kumuandalia Rebeca chakula cha usiku. Je, Ibrahim anataka kuandaa chakula cha mchana kwa ajili ya Rebeca? Hapana, Ibrahim hataki kuandaa chakula cha mchana kwa ajili ya Rebeca. Anataka kumuandalia chakula cha usiku.
3) Ibrahim anaenda katika duka la vyakula kununua vyakula. Je, Ibrahim alienda katika duka la vyakula? Ndiyo, Ibrahim alienda katika duka la vyakula kununua vyakula.
4) Ibrahim anatembea kupita safu ya mboga za majani. Je, Ibrahim alinunua mboga za majani? Hapana, Ibrahim hakununua mboga za majani. Alitembea kupita safu ya mboga za majani.
5) Ibrahim anaangalia samaki ndani ya friji, lakini hakununua yoyote. Je, Ibrahim aliangalia samaki? Ndiyo, Ibrahim aliangalia samaki ndani ya friji, lakini hakununua yoyote.
6) Ibrahim mwisho anaondoka dukani humo na kwenda nyumbani. Je, Ibrahim alibaki dukani? Hapana, Ibrahim mwisho aliondoka dukani na kwenda nyumbani.
7) Ibrahim anaagiza piza badala yake. Je, Ibrahim aliandaa chakula cha usiku? Hapana, Ibrahim hakuandaa chakula cha usiku. Aliagiza piza badala yake.