×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

LingQ Mini Stories, 8- Ninataka Kununua Viatu Vipya – Text to read

LingQ Mini Stories, 8- Ninataka Kununua Viatu Vipya

Iniciante 1 Suaíli lesson to practice reading

Comece a aprender esta lição agora

Vailet anataka kununua viatu vipya.

Anaenda ndani ya duka la viatu.

Kuna viatu vingi vizuri hapo.

Vailet anajaribu kuvaa jozi ya viatu vya bluu.

Viatu vya bluu vinambana sana.

Anajaribu kuvaa jozi ya viatu vyeusi.

Viatu hivi vinamkaa vizuri sana.

Vailet anauliza gharama ya viatu vile vyeusi.

Viatu vyeusi ni shilingi laki mbili na elfu hamsini.

Vailet kwa huzuni anaviweka viatu vile chini na kuondoka.

Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na Vailet

Ninataka kununua viatu vipya.

Ninaenda ndani ya duka la viatu.

Kuna viatu vingi vizuri hapo.

Ninajaribu kuvaa jozi ya viatu vya bluu.

Viatu vya bluu vinanibana sana.

Ninajaribu jozi ya viatu vyeusi.

Viatu hivi vinanikaa vizuri sana.

Ninauliza gharama ya viatu vile vyeusi.

Viatu vyeusi ni shilingi laki mbili na elfu hamsini.

Kwa huzuni naviweka viatu vile chini na kuondoka.

Maswali.

1) Vailet anataka kununua viatu vipya. Je, Vailet anataka kununua viatu vipya? Ndiyo, Vailet anataka kununua viatu vipya.

2) Kuna viatu vingi vizuri ndani ya duka la viatu. Je, kuna viatu vingi ndani ya duka la viatu? Ndiyo, kuna viatu vingi vizuri ndani ya duka la viatu.

3) Vailet anajaribu kuvaa jozi ya viatu vya blue na vyeusi. Je, Vailet amejaribu jozi mbili ya viatu? Ndiyo, Vailet amejaribu jozi mbili ya viatu. Amejaribu kuvaa jozi ya bluu na nyeusi.

4) Kwanza, Vailet amejaribu jozi ya viatu vya bluu. Je, Vailet amejaribu jozi ya viatu vyekundu kwanza? Hapana, Vailet hajajaribu jozi ya viatu vyekundu. Amejaribu jozi ya viatu vya bluu.

5) Viatu vya bluu vinambana sana. Je, viatu vya bluu vinamkaa vizuri? Hapana, viatu vya bluu havimkai vizuri. Vinambana sana.

6) Viatu vyeusi vinamkaa vizuri. Je, viatu vyeusi vinamkaa vizuri? Ndiyo, viatu vyeusi vinamkaa vizuri.

7) Viatu vyeusi ni shilingi laki mbili na elfu hamsini. Je, viatu vyeusi vina gharama kubwa? Ndiyo, viatu vyeusi vina gharama kubwa. Ni shilingi laki mbili na elfu hamsini.

8) Vailet anaweka chini viatu na kuondoka dukani. Je, Vailet alinunua viatu? Hapana, Vailet hakununua viatu. Aliviweka chini na kuondoka dukani.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE