×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

image

LingQ Mini Stories, 40 - Wanini Ana Familia Kubwa

Wanini ana watu wengi katika familia yake.

Ana kaka, dada, na binamu wengi.

Ndugu ya Wanini ni mkubwa kuliko Wanini.

Yeye pia ana sauti na mcheshi kuliko Wanini.

Dada ya Wanini ni mdogo kuliko Wanini.

Dada ya Wanini pia ni mfupi na mwenye urafiki zaidi.

Dadake Wanini anapenda kuongea na watu kuliko Wanini.

Ingawa Wanini ana binamu wengi wakubwa, yeye hawafahamu vizuri sana.

Wanaishi mbali zaidi kuliko kaka na dada yake.

Hapa kuna hadithi sawa iliyosimuliwa kwa njia tofauti.

Nina watu wengi katika familia yangu.

Nina kaka, dada, na binamu wengi.

Ndugu yangu ni mkubwa kuniliko.

Yeye ana sauti na ucheshi kuniliko.

Dada yangu ni mdogo kuniliko.

Dada yangu pia ni mfupi na mwenye urafiki zaidi.

Dada yangu anapenda kuzungumza na watu zaidi kuniliko.

Ingawa nina binamu wengi wakubwa, siwafahamu vizuri.

Wanaishi mbali zaidi kuliko kaka na dada yangu.

Maswali:

Moja: Wanini ana watu wengi katika familia yake.

Je, Wanini ana familia kubwa? Ndiyo, Wanini ana watu wengi katika familia yake.

Mbili: Wanini ana kaka mmoja.

Je, Wanini ana ndugu wangapi? Ana kaka mmoja.

Tatu: Kaka yake Wanini ni mkubwa kumliko.

Nani mkubwa, Wanini au kaka yake? Ndugu ya Wanini ni mkubwa kumliko.

Nne: Ndugu ya Wanini ana sauti zaidi kumliko.

Ni mtu gani mwenye sauti zaidi, Wanini au kaka yake? Ndugu ya Wanini ana sauti zaidi kumliko.

Tano: Dada ya Wanini ni mdogo kumliko.

Nani mdogo, Wanini au dada yake? Dada ya Wanini ni mdogo kumliko.

Sita: Dada ya Wanini ni mkarimu zaidi kuliko Wanini, kwa hivyo anapenda kuzungumza na watu zaidi.

Ni mtu gani anapenda kuzungumza na watu zaidi, Wanini au dada yake?

Dada ya Wanini ni mkarimu zaidi kuliko Wanini, kwa hivyo anapenda kuzungumza na watu zaidi ya Wanini.

Saba: Wanini ana binamu wengi wakubwa.

Je, Wanini ana binamu wachache? Hapana, Wanini ana binamu wengi wakubwa.

Nane: Kaka na dada ya Wanini wanaishi karibu zaidi kuliko binamu zake.

Ni nani anayeishi karibu zaidi, binamu za Wanini, au kaka na dada yake? Kaka na dada ya Wanini wanaishi karibu zaidi kuliko binamu zake.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE