×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

LingQ Mini Stories, 2- Sikukuu za Majira ya Baridi Kali – Text to read

LingQ Mini Stories, 2- Sikukuu za Majira ya Baridi Kali

Iniciante 1 Suaíli lesson to practice reading

Comece a aprender esta lição agora

David ana msisimko kwa ajili ya sikukuu za majira ya baridi kali.

Ana likizo majira ya baridi kali.

Haitajiki kufanya kazi kwa wiki mbili.

Anataka kwenda kwenye mapumziko.

Lakini, hajui aende wapi.

Anataka kwenda Ufaransa.

Lakini Ufaransa ni gharama.

Tiketi za ndege zina bei kubwa.

Na David hajui kuongea Kifaransa.

Anaamua kusoma, kutunza pesa, na kubaki nyumbani.

Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na David.

Nina msisimko kwa ajili ya sikukuu za majira ya baridi kali.

Nina likizo majira ya baridi kali.

Sihitajiki kufanya kazi kwa wiki mbili.

Nataka kwenda kwenye mapumziko.

Lakini, sijui niende wapi.

Ninataka kwenda Ufaransa.

Lakini Ufaransa ni gharama.

Tiketi za ndege zina bei kubwa.

Na sijui kuongea Kifaransa.

Ninaamua kusoma, kutunza pesa, na kubaki nyumbani.

Maswali:

1) David ana msisimko kwa ajili ya sikukuu za majira ya baridi kali. Je, David ana msisimko? Ndiyo, David ana msisimko kwa ajili ya sikukuu za majira ya baridi kali.

2) David ana likizo majira ya baridi kali. Je, David ana muda wa ziada kipindi cha majira ya baridi kali? Ndiyo, David ana likizo majira ya baridi kali.

3) David anataka kwenda kwenye mapumziko. Je, David anataka kubaki nyumbani? Hapana, David hataki kubakia nyumbani. Anataka kwenda kwenye mapumziko.

4) David hajui aende wapi. Je, David anajua wapi aende? Hapana, David hajui wapi aende.

5) David anataka kwenda Ufaransa kwa mapumziko. Je, David anataka kwenda Ufaransa? Ndiyo, David anataka kwenda Ufaransa kwa ajili ya mapumziko yake.

6) Ufaransa ni gharama. Je, Ufaransa ni bei rahisi? Hapana, Ufaransa sio bei rahisi. Ufaransa ni gharama.

7) David hajui kuongea Kifaransa. Je, David huwa anaongea Kifaransa? Hapana, David hajui kuongea Kifaransa.

8) David ameamua kusoma Kifaransa, kutunza pesa, na kubakia nyumbani kwa mapumziko. Je, David ameamua kusoma Kifaransa? Ndiyo, ameamua kusoma Kifaransa, kutunza pesa, na kubakia nyumbani kwa mapumziko.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE