×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

image

LingQ Mini Stories, 19- Ninaenda Katika Mgahawa

Darasa la hisabati limemalizika muda sio mrefu.

Ni mchana na ni muda wa chakula cha mchana.

Barnaba hakuja na chakula chake cha mchana kutoka nyumbani.

Inabidi anunue chakula cha mchana shuleni.

Anaenda katika mgahawa.

Anaona biskuti za chokoleti, na saladi.

Mama yake anataka ale saladi.

Lakini Barnaba anataka kula biskuti za chokoleti

Anafikiria kwa dakika.

Kisha, ananunua biskuti na kuzila.

Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Barnaba.

Darasa la hisabati limemalizika muda sio mrefu.

Ni mchana na ni muda wa chakula cha mchana.

Sikuja na chakula cha mchana kutoka nyumbani.

Inabidi ninue chakula cha mchana shuleni.

Ninaenda katika mgahawa.

Ninaona biskuti za chokoleti, na saladi.

Mama yangu anataka nile saladi.

Lakini mimi ninataka kula biskuti za chokoleti.

Ninafikiria kwa dakika.

Kisha, ninanunua biskuti na kuzila.

Maswali.

1) Darasa la hesabu la Barnaba limemalizika muda sio mrefu. Je, darasa la hesabu limeanza muda sio mrefu? Hapana, darasa la hesabu halijaanza. Limemalizika muda sio mrefu.

2) Ni mchana na ni muda wa chakula cha mchana. Je, ni muda wa chakula cha mchana? Ndiyo, ni muda wa chakula cha mchana. Ni mchana.

3) Barnaba hakuja na chakula cha mchana. Je, Barnaba alikuja na chakula cha mchana? Hapana, Barnaba hakuja na chakula cha mchana.

4) Anaenda katika mgahawa. Je, Barnaba anaenda nyumbani kula chakula cha mchana? Hapana, Barnaba haendi nyumbani. Anaenda katika mgahawa.

5) Barnaba anaona saladi na biskuti za chokoleti ndani ya mgahawa. Je, Barnaba anaona saladi? Ndiyo, Barnaba anaona saladi na biskuti za chokoleti ndani ya mgahawa.

6) Mama yake anataka ale saladi, siyo biskuti za chokoleti. Je, mama yake Barnaba anataka yeye ale saladi? Ndiyo, mama yake anataka ale saladi, sio biskuti za chokoleti.

7) Barnaba ananunua biskuti. Je, Barnaba ananunua saladi? Hapana, Barnaba hanunui saladi. Ananunua biskuti na kuzila.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE