Aisha huwa anapenda kusikiliza muziki.
Anataka kujifunza namna ya kucheza.
Anaenda katika darasa lake la kwanza la kucheza.
Mwalimu anamwambia anyooshe miguu yake.
Aisha anajaribu kunyoosha miguu yake.
Lakini hawezi kunyoosha mbali sana.
Mwalimu anamwambia aruke.
Aisha anajaribu kuruka, lakini anadondoka chini.
Misuli ya Aisha ina maumivu baada ya darasa.
Labda hawezi kujifunza namna ya kucheza.
Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Aisha.
Huwa ninapenda kusikiliza muziki.
Ninataka kujifunza namna ya kucheza.
Ninaenda katika darasa langu la kwanza la kucheza.
Mwalimu ananiambia ninyooshe miguu yangu.
Ninajaribu kunyoosha miguu yangu.
Lakini siwezi kunyoosha mbali sana.
Mwalimu ananiambia niruke.
Ninajaribu kuruka, lakini ninadondoka chini.
Misuli yangu ina maumivu baada ya darasa.
Labda siwezi kujifunza namna ya kucheza.
Maswali.
1) Aisha huwa anapenda kusikiliza muziki. Je, Aisha anapenda muziki? Ndiyo, Aisha huwa anapenda kusikiliza muziki.
2) Aisha anataka kujifunza namna ya kucheza. Je, Aisha anataka kujifunza namna ya kucheza? Ndiyo, Aisha anataka kujifunza namna ya kucheza.
3) Aisha anaenda kwenye darasa la kucheza. Je, Aisha anaenda kwenye darasa la kinanda? Hapana, Aisha hajaenda kwenye darasa la kinanda. Anaenda kwenye darasa la kucheza.
4) Mwalimu anamwambia Aisha anyooshe miguu yake. Je, mwalimu anamwambia Aisha anyooshe mikono yake? Hapana, mwalimu hamwambii anyooshe mikono yake. Mwalimu anamwambia kunyoosha miguu yake.
5) Aisha hawezi kunyoosha miguu yake mbali sana. Je, Aisha anaweza kunyoosha miguu yake mbali? Hapana, Aisha hawezi kunyoosha miguu yake mbali sana.
6) Aisha anajaribu kuruka, lakini anadondoka chini. Je, Aisha anadondoka chini? Ndiyo, Aisha anajaribu kuruka, lakini anadondoka chini.
7) Misuli ya Aisha ina maumivu baada ya darasa. Je, misuli ya Aisha ina maumivu baada ya darasa? Ndiyo, misuli ya Aisha ina maumivu baada ya darasa.
8) Labda Aisha hawezi kujifunza kucheza. Je, Aisha anaweza kujifunza kucheza? Labda Aisha hawezi kujifunza kucheza.