×

Nós usamos os cookies para ajudar a melhorar o LingQ. Ao visitar o site, você concorda com a nossa política de cookies.

LingQ Mini Stories, 11- Nyumba Yangu Ni Ndogo Sana – Texto para ler

LingQ Mini Stories, 11- Nyumba Yangu Ni Ndogo Sana

Iniciante 1 lição de Suaíli para praticar a leitura

Comece a aprender esta lição agora

Nyumba ya Jumanne ni ndogo sana.

Anataka kuhamia nyumba mpya.

Anatazama picha za nyumba kwenye intaneti.

Nyumba moja ni bei nafuu sana.

Ila imezeeka na ipo tupu.

Nyumba nyingine ina samani ndani yake.

Ina kitanda, televisheni, na jiko.

Ila, hiyo nyumba ni gharama.

Jumanne anaamua kutunza fedha zaidi.

Namna hiyo, ataweza kuhama mwaka ujao.

Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Jumanne.

Nyumba yangu ni ndogo sana.

Ninataka kuhamia kwenye nyumba mpya.

Ninatazama picha za nyumba kwenye intaneti.

Nyumba moja ni bei rahisi.

Lakini imezeeka na ni tupu.

Nyumba nyingine ina samani ndani yake.

Ina kitanda, televisheni, na jiko.

Ila, nyumba hiyo ni gharama.

Ninaamua kutunza fedha zaidi.

Namna hiyo, nitaweza kuhama mwaka ujao.

Maswali.

1) Nyumba ya Jumanne ni ndogo sana. Je, nyumba ya Jumanne ni kubwa? Hapana, nyumba yake sio kubwa. Ni ndogo sana.

2) Jumanne anataka kuhamia kwenye nyumba mpya. Je, Jumanne anataka kuhama? Ndiyo, Jumanne anataka kuhamia kwenye nyumba mpya.

3) Jumanne anatazama picha za nyumba kwenye intaneti. Je, Jumanne anatazama picha za magari? Hapana, Jumanne hatazami picha za magari. Anatazama picha za nyumba.

4) Nyumba ya kwanza ni bei nafuu. Je, nyumba ya kwanza ni gharama? Hapana, nyumba ya kwanza sio gharama. Ni bei nafuu.

5) Nyumba ya kwanza imezeeka na ipo tupu. Je, nyumba ya kwanza imezeeka? Ndiyo, nyumba ya kwanza imezeeka na ipo tupu.

6) Nyumba nyingine ina kitanda, televisheni, na jiko. Je, nyumba nyingine ina samani? Ndiyo, nyumba nyingine ina kitanda, televisheni, na jiko.

7) Nyumba yenye samani ni gharama. Je, nyumba yenye samani ni bei nafuu? Hapana, nyumba yenye samani sio bei nafuu, ni gharama.

8) Jumanne anaamua kutunza fedha zaidi. Je, Jumanne anataka kutunza fedha zaidi? Ndiyo, Jumanne anaamua kutunza fedha zaidi.

9) Jumanne anaweza kuhama mwaka ujao. Je, Jumanne anaweza kuhama mwaka huu? Hapana, Jumanne hawezi kuhama mwaka huu. Anaweza kuhama mwaka ujao.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE