×

우리는 LingQ를 개선하기 위해서 쿠키를 사용합니다. 사이트를 방문함으로써 당신은 동의합니다 쿠키 정책.


image

Storybooks Canada, Khalai azungumza na mimea

Khalai azungumza na mimea

https://storybookscanada.ca/images/0089/02.jpg" alt="A girl in a field waving."/>

Khalai ni msichana mwenye umri wa miaka saba. Jina lake lina maana ya ‘aliye mzuri' katika lugha yake ya Lubukusu.

https://storybookscanada.ca/images/0089/03.jpg" alt="A girl talking to an orange tree."/>

Khalai anaamka na kuongea na mmea mchanga wa Mchungwa, “Tafadhali mti wa Mchungwa, kua mkubwa uzae machungwa mengi mabivu.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/04.jpg" alt="A girl kneeling on the ground talking to grass."/>

Khalai anaenda shuleni na njiani anaongea na Nyasi, “Tafadhali Nyasi, kua kijani zaidi na zaidi na wala usikauke.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/05.jpg" alt="A girl looking at wild flowers."/>

Khalai anayapita Maua ya mwituni na kusema, “Tafadhali Maua, endelea kunawiri ili niweze kukuweka kwenye nywele zangu.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/06.jpg" alt="A girl next to a tree in a school playground."/>

Akiwa shuleni, Khalai anazunguumza na Mti ulioko katikati ya shule, “Tafadhali Mti, toa matawi makubwa ili tusome chini ya kivuli chako.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/07.jpg" alt="A girl talking to a hedge outside a school."/>

Khalai anazunguumza na ua unaoizingira shule yake, “Tafadhali ua, kuwa mwenye nguvu ili uzuie shule yetu kutokana na watu wabaya.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/08.jpg" alt="A girl next to an orange tree."/>

Anaporudi nyumbani alasiri, Khalai anautembelea mti wa Mchungwa kuangalia kama machungwa yameiva.

https://storybookscanada.ca/images/0089/09.jpg" alt="A girl next to an orange tree."/>

“Machungwa bado mabichi,” Khalai anashusha pumzi. “Nitakuona kesho, we mti wa machungwa. Labda utanipa chungwa bivu wakati huo.”

Khalai azungumza na mimea Khalai spricht mit Pflanzen Khalai talks to plants Khalai parle aux plantes 칼라이는 식물과 이야기를 나눈다 Khalai bitkilerle konuşuyor

A girl in a field waving.

Khalai ni msichana mwenye umri wa miaka saba. Jina lake lina maana ya ‘aliye mzuri' katika lugha yake ya Lubukusu. Khalai is a seven-year-old girl. His name means 'the good one' in his Lubukusu language. Khalai est une fillette de sept ans. Son nom signifie « le bon » dans sa langue Lubukusu.

A girl talking to an orange tree.

Khalai anaamka na kuongea na mmea mchanga wa Mchungwa, “Tafadhali mti wa Mchungwa, kua mkubwa uzae machungwa mengi mabivu.” Khalai wakes up and talks to the young Orange plant, "Please Orange tree, big tree, produce many ripe oranges." Khalai se réveille et parle au jeune plant d'oranger : « S'il vous plaît Oranger, grand arbre, produisez beaucoup d'oranges mûres.

A girl kneeling on the ground talking to grass.

Khalai anaenda shuleni na njiani anaongea na Nyasi, “Tafadhali Nyasi, kua kijani zaidi na zaidi na wala usikauke.” Khalai goes to school and on the way he talks to Grass, "Please Grass, grow greener and greener and don't dry up."

A girl looking at wild flowers.

Khalai anayapita Maua ya mwituni na kusema, “Tafadhali Maua, endelea kunawiri ili niweze kukuweka kwenye nywele zangu.” Khalai walks past Wild Flowers and says, "Please Flowers, keep blooming so I can put you in my hair." Khalai passe devant Wild Flowers et dit : "S'il te plaît, Flowers, continue de fleurir pour que je puisse te mettre dans mes cheveux."

A girl next to a tree in a school playground.

Akiwa shuleni, Khalai anazunguumza na Mti ulioko katikati ya shule, “Tafadhali Mti, toa matawi makubwa ili tusome chini ya kivuli chako.” While at school, Khalai talks to the Tree in the middle of the school, "Please Tree, give big branches so that we can study under your shade." À l'école, Khalai parle à l'arbre au milieu de l'école : « S'il te plaît, arbre, donne de grosses branches pour que nous puissions étudier sous ton ombre.

A girl talking to a hedge outside a school.

Khalai anazunguumza na ua unaoizingira shule yake, “Tafadhali ua, kuwa mwenye nguvu ili uzuie shule yetu kutokana na watu wabaya.” Khalai talks to the fence that surrounds his school, "Please fence, be strong to protect our school from bad people." Khalai parle à la clôture qui entoure son école : « S'il vous plaît, clôturez, soyez forts pour protéger notre école des mauvaises personnes. »

A girl next to an orange tree.

Anaporudi nyumbani alasiri, Khalai anautembelea mti wa Mchungwa kuangalia kama machungwa yameiva. When he returns home in the afternoon, Khalai visits the orange tree to check if the oranges are ripe.

A girl next to an orange tree.

“Machungwa bado mabichi,” Khalai anashusha pumzi. “Nitakuona kesho, we mti wa machungwa. Labda utanipa chungwa bivu wakati huo.” "The oranges are still fresh," Khalai sighs. "I'll see you tomorrow, orange tree. Maybe you'll give me a ripe orange then." "Les oranges sont encore fraîches", soupire Khalai. "Je te verrai demain, oranger. Peut-être que tu me donneras une orange mûre alors."