×

Usamos cookies para ayudar a mejorar LingQ. Al visitar este sitio, aceptas nuestras politicas de cookie.

LingQ Mini Stories, 13- Nina Miadi Na Rajabu – Text to read

LingQ Mini Stories, 13- Nina Miadi Na Rajabu

Principiante 1 Suajili lesson to practice reading

Comienza a aprender esta lección ya

Latifa yupo ndani ya mgahawa.

Ana miadi na Rajabu.

Latifa hamjui Rajabu.

Lakini ni rafiki wa rafiki yake.

Rajabu anakuja ndani ya muda, na anasema "Habari!"

Anauliza, "Wewe ni Rajabu? Mimi ni Latifa."

Rajabu anakaa chini, na Latifa anamtizama.

Anawaza kuwa ni mtanashati sana.

Latifa anatabasamu, na Rajabu anamtazama.

"Una tabasamu zuri." Rajabu akasema.

Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Latifa.

Nipo ndani ya mgahawa.

Nina miadi na Rajabu.

Simjui Rajabu.

Lakini ni rafiki wa rafiki yangu.

Anakuja ndani ya muda, na anasema "Habari!"

Ninamuuliza, "Wewe ni Rajabu? Mimi ni Latifa."

Anakaa chini, na ninamtizama.

Ninawaza kuwa ni mtanashati sana.

Ninatabasamu, na Rajabu ananitazama.

"Una tabasamu zuri." Rajabu akasema.

Maswali:

1) Latifa yupo katika mgahawa. Je, Latifa yupo nyumbani? Hapana, Latifa hayupo nyumbani. Yupo katika mgahawa.

2) Latifa ana miadi na Rajabu. Je, Latifa ana miadi na Nathan? Hapana, Latifa hana miadi na Nathan. Ana miadi na Rajabu.

3) Latifa hamjui Rajabu, lakini ni rafiki wa rafiki yake. Je, Latifa anamjua Rajabu? Hapana, Latifa hamjui Rajabu, lakini ni rafiki wa rafiki yake.

4) Rajabu anakuja kwenye mgahawa ndani ya muda. Je, Rajabu amechelewa? Hapana, Rajabu hajachelewa. Amefika katika mgahawa ndani ya muda.

5) Rajabu anasema "Habari!" kwa Latifa. Je, Rajabu anasema lolote kwa Latifa? Ndiyo, Rajabu anasema "Habari!" kwa Latifa.

6) Latifa anamuuliza Rajabu kama yeye ni Rajabu. Je, Latifa anamuuliza Rajabu swali? Ndiyo, Latifa anamuuliza Rajabu kama yeye ni Rajabu.

7) Latifa anawaza kwamba Rajabu ni mtanashati. Je, Latifa anawaza Rajabu ni mtanashati? Ndiyo, Latifa anawaza Rajabu ni mtanashati.

8) Rajabu anasema Latifa ana tabasamu zuri. Je, Rajabu anapenda tabasamu la Latifa? Ndiyo, Rajabu anasema Latifa ana tabasamu zuri.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE