×

我們使用cookies幫助改善LingQ。通過流覽本網站,表示你同意我們的 cookie 政策.

Who is She?, 23- Siri Ni Nini? — 閱讀文本

Who is She?, 23- Siri Ni Nini?

初級1 斯瓦希里語 課程,練習閱讀

立即開始學習本課

Hivyo mtu anaweza tu akalala kitandani cha mtu mwingine wakati amechoka?

Hapaswi kuomba ruhusa?

Hakukuwa na yeyote wa kuuliza.

Mbona inakusumbua sana?

Je, wewe ni mpenzi wa Ibrahim?

Hio ndiyo sababu?

Hapana, mimi sio mpenzi wa Ibrahim, kama ungependa kujua.

Mimi ni mwanafunzi wa lugha wa Ibrahim.

Unanitania?

Wewe ni mwanafunzi wa lugha wa Ibrahim?

Huwezi nindanganya.

Hapana, ni kweli.

Ibrahim amekuwa akinisaidia kujifunza Kiingereza.

Lakini unazungumza Kiingereza vizuri.

Siamini wewe ni mwanafunzi wake.

Naam kwa hakika.

Au tuseme, nilikuwa.

Nilipofika hapa kwanza, sikuweza kuzungumza vizuri sana.

Na kwa kuishi tu na Ibrahim, umejifunza kuongea vizuri?

Alikusaidia sana hivyo?

Sio tu kuzungumza vizuri, pia naandika vizuri, na si shida kusoma vitabu vigumu.

Ulijifunzaje?

Siri ni nini?

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE