×

我們使用cookies幫助改善LingQ。通過流覽本網站,表示你同意我們的 cookie 政策.

LingQ Mini Stories, 3- Naomi Alinunua Paka — 閱讀文本

LingQ Mini Stories, 3- Naomi Alinunua Paka

初級1 斯瓦希里語 課程,練習閱讀

立即開始學習本課

Naomi ameboreka kazini na nyumbani.

Huwa anafanya kitu kile kile kila siku.

Anataka fani mpya.

Kwanza, amejaribu kupika.

Lakini chakula chake huwa hakina ladha nzuri.

Kisha, amejaribu kuogelea.

Lakini anaogopa maji.

Naomi anatembea kuelekea nyumbani na akaona duka la wanyama wa kufugwa.

Ndani ya duka la wanyama wa kufugwa, akaona paka!

Naomi akamnunua huyo paka, na sasa ana furaha sana.

Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na Naomi.

Nimeboreka kazini na nyumbani.

Huwa ninafanya kitu kile kile kila siku.

Ninataka fani mpya.

Kwanza, nimejaribu kupika.

Lakini chakula changu huwa hakina ladha nzuri.

Kisha, nimejaribu kuogelea.

Lakini naogopa maji.

Nikielekea nyumbani nikaona duka la wanyama wa kufugwa.

Ndani ya duka la wanyama wa kufugwa, nikaona paka!

Nikanunua huyo paka, na sasa nina furaha sana.

Maswali:

1) Naomi ameboreka kazini, na nyumbani. Je, Naomi anafuraha kazini? Hapana, Naomi hana furaha kazini. Ameboreka kazini, na nyumbani.

2) Naomi huwa anafanya kitu kile kile kila siku. Je, Naomi huwa anafanya vitu vingi vipya? Hapana, Naomi huwa anafanya kitu kile kile kila siku.

3) Naomi anataka fani mpya. Je, Naomi anataka fani mpya? Ndiyo, Naomi anataka fani mpya.

4) Chakula cha Naomi huwa hakina ladha nzuri. Je, Naomi ni mpishi mzuri? Hapana, Naomi sio mpishi mzuri. Chakula chake huwa hakina ladha nzuri.

5) Naomi anaogopa maji. Je, Naomi anapenda kuogelea? Hapana, Naomi hapendi kuogelea. Anaogopa maji.

6) Naomi anaona paka ndani ya duka la wanyama wa kufugwa. Je, Naomi anaona paka ndani ya duka? Ndiyo, Naomi anaona paka ndani ya duka la wanyama wa kufugwa.

7) Naomi alinunua paka kutoka kwenye duka la wanyama wa kufugwa. Je, Naomi alinunua paka? Ndiyo, Naomi alinunua paka kutoka kwenye duka la wanyama wa kufugwa.

8) Naomi sasa ana furaha sana kwa sababu ana paka. Je, Naomi ameboreka sasa? Hapana, Naomi hajaboreka. Sasa ana furaha sana kwa sababu ana paka.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE