×

我們使用cookies幫助改善LingQ。通過流覽本網站,表示你同意我們的 cookie 政策.

LingQ Mini Stories, 18- Hajui Avae Nini — 閱讀文本

LingQ Mini Stories, 18- Hajui Avae Nini

初級1 斯瓦希里語 課程,練習閱讀

立即開始學習本課

Happy anajiandaa asubuhi.

Hajui avae nini.

Anatazama ndani ya kabati lake la nguo.

Anaona sketi ya kahawia.

Lakini kuna baridi sana leo.

Anaona jozi ya suruali nyeusi sakafuni.

Lakini ni chafu kidogo.

Na ana kikao kazini leo.

Happy anavaa sketi ya kahawia.

Inampendeza, lakini miguu yake ni ya baridi.

Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Happy.

Ninajiandaa asubuhi.

Sijui nivae nini.

Ninatazama ndani ya kabati langu la nguo.

Ninaona sketi ya kahawia.

Lakini kuna baridi sana leo.

Ninaona jozi ya suruali nyeusi sakafuni.

Lakini ni chafu kidogo.

Na nina kikao kazini leo.

Ninavaa sketi ya kahawia.

Inanipendeza, lakini miguu yangu ni ya baridi.

Maswali.

1) Happy anajiandaa asubuhi. Je, Happy anajiandaa usiku? Hapana, hajiandai usiku. Anajiandaa asubuhi.

2) Happy hajui avae nini. Je, Happy anajua avae nini? Hapana, hajui avae nini.

3) Happy anatazama ndani ya kabati lake la nguo ili kuona kitu cha kuvaa. Je, Happy anatazama chini ya kitanda? Hapana, Happy hatazami chini ya kitanda. Anatazama ndani ya kabati la nguo.

4) Kuna sketi ya kahawia ndani ya kabati la nguo. Je, kuna sketi ya kahawia ndani ya kabati la nguo? Ndiyo, kuna sketi ya kahawia ndani ya kabati la nguo.

5) Kuna baridi sana leo. Je, kuna joto leo? Hapana, hakuna joto leo. Kuna baridi sana.

6) Happy anaona jozi ya suruali nyeusi sakafuni. Je, suruali zipo kitandani? Hapana, suruali hazipo kitandani. Zipo sakafuni.

7) Happy ana kikao kazini leo. Je, Happy ana kikao leo? Ndiyo, Happy ana kikao kazini leo.

8) Happy anavaa sketi ya kahawia. Je, Happy anavaa suruali nyeusi? Hapana, Happy hajavaa suruali. Anavaa sketi ya kahawia.

9) Miguu ya Happy ni ya baridi kwa sababu amevaa sketi. Je, miguu ya Happy ni ya baridi? Ndiyo, miguu ya Happy ni ya baridi kwa sababu amevaa sketi.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE