×

我們使用cookies幫助改善LingQ。通過流覽本網站,表示你同意我們的 cookie 政策.

LingQ Mini Stories, 15- Eliza Hana Nguvu — 閱讀文本

LingQ Mini Stories, 15- Eliza Hana Nguvu

初級1 斯瓦希里語 課程,練習閱讀

立即開始學習本課

Johari na Eliza wanataka kupunguza uzito.

Wanataka kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi.

Ila kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ni gharama.

Hivyo wanaamua kufanya mazoezi nyumbani.

Johari anaanza kukimbia, na Eliza ananyanyua vyuma.

Ila Johari hapendi kukimbia.

Na Eliza hana nguvu.

Na pia wametingwa sana na kazi.

Hawana muda wa kufanya mazoezi.

Labda watajaribu tena wiki ijayo.

Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Johari.

Eliza na mimi tunataka kupunguza uzito.

Tunataka kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi.

Ila kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ni gharama.

Hivyo, tunaamua kufanya mazoezi nyumbani.

Ninaanza kukimbia, na Eliza anaanza kunyanyua vyuma.

Ila sipendi kukimbia.

Na Eliza hana nguvu.

Pia tumetingwa sana na kazi.

Hatuna muda wa kufanya mazoezi.

Labda tutajaribu tena wiki ijayo.

Maswali.

1) Johari na Eliza wanataka kufanya mazoezi kwenye ukumbi wa mazoezi. Je, Johari na Eliza wanataka kufanya mazoezi? Ndiyo, wanataka kufanya mazoezi kwenye ukumbi wa mazoezi.

2) Kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ni gharama. Je, kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ni bei rahisi? Hapana, sio bei rahisi. Kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ni gharama.

3) Wanaamua kufanya mazoezi nyumbani, sababu ukumbi wa mazoezi ni gharama sana. Je, ukumbi wa mazoezi ni upo mbali sana nao? Hapana, ukumbi wa mazoezi haupo mbali sana nao. Ukumbi wa mazoezi ni gharama sana.

4) Johari hapendi kukimbia. Je Johari anapenda kukimbia? Hapana, Johari hapendi kukimbia.

5) Eliza anajaribu kunyanyua vyuma, lakini hana nguvu. Je, Eliza anajaribu kukimbia pia? Hapana, Eliza hajajaribu kukimbia. Anajaribu kunyanyua vyuma.

6) Eliza hana nguvu. Je, Eliza ana nguvu za kutosha kunyanyua vyuma? Hapana, Eliza hana nguvu.

7) Johari na Eliza wametingwa sana na kazi, hivyo hawana muda mwingi wa kufanya mazoezi. Je, Johari na Eliza wametingwa sana na kazi? Ndiyo, wametingwa sana na kazi, hawana muda mwingi wa kufanya mazoezi.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE