×

我們使用cookies幫助改善LingQ。通過流覽本網站,表示你同意我們的 cookie 政策.

LingQ Mini Stories, 10- Sherehe Ya Kuzaliwa — 閱讀文本

LingQ Mini Stories, 10- Sherehe Ya Kuzaliwa

初級1 斯瓦希里語 課程,練習閱讀

立即開始學習本課

William anaenda kwenye sherehe ya kuzaliwa.

Anahitaji kununua zawadi kwa ajili ya Eva.

Ila, William huwa haendi katika sherehe nyingi.

Ana wasiwasi na anajiuliza anunue nini.

Eva huwa anapenda vito, wanyama, na rangi ya bluu.

William anaenda katika duka la vito.

Anaona mkufu mzuri wa fedha.

Mkufu huo una paka wa bluu juu yake.

William anafurahi, na ananunua mkufu huo.

Anatarajia Eva ataupenda mkufu huo.

Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na William.

Ninaenda kwenye sherehe ya kuzaliwa.

Ninahitaji kununua zawadi kwa ajili ya Eva.

Ila, huwa siendi kwenye sherehe nyingi sana.

Nina wasiwasi na ninajiuliza ninunue nini.

Eva huwa anapenda vito, wanyama, na rangi ya bluu.

Ninaenda kwenye duka la vito.

Ninaona mkufu mzuri wa fedha.

Mkufu huo una paka wa bluu juu yake.

Ninafurahi, na kununua mkufu huo.

Ninatarajia Eva ataupenda mkufu huo.

Maswali.

1) William anaenda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Eva. Je, William anaenda kwenye sherehe ya kuzaliwa? Ndiyo, William anaenda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Eva.

2) William huwa haendi kwenye sherehe nyingi, hivyo anajisikia wasiwasi. Je, William huwa anaenda kwenye sherehe nyingi? Hapana, William huwa haendi kwenye sherehe nyingi, hivyo anajisikia wasiwasi.

3) Eva anapenda wanyama, na rangi ya bluu. Je, Eva anapenda wanyama? Ndiyo, Eva anapenda wanyama, na pia anapenda rangi ya bluu.

4) William anaenda katika duka la vito. Je, Eva alienda katika duka la vito? Hapana, Eva hakwenda katika duka la vito, lakini William alikwenda.

5) William anaona mkufu wa fedha. Je, William aliona pete? Hapana, aliona mkufu wa fedha, sio pete.

6) Mkufu ni wa fedha. Je mkufu ni wa fedha, au dhahabu? Mkufu ni wa fedha, sio wa dhahabu.

7) Kuna paka wa bluu kwenye mkufu. Je, kuna paka wa zambarau kwenye mkufu? Hapana, hakuna. Kuna paka wa bluu kwenye mkufu.

8) William ananunua mkufu kwa sababu anatarajia Eva ataupenda. Je, William ananunua mkufu? Ndiyo, William ananunua mkufu kwa sababu anatarajia Eva ataupenda.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE