×

我们使用 cookie 帮助改善 LingQ。通过浏览本网站,表示你同意我们的 cookie 政策.

Habari za UN, Methali: Aanguae huanguliwa | | Habari za UN – 阅读文本

Habari za UN, Methali: Aanguae huanguliwa | | Habari za UN

中级2 斯瓦希里语 课程,练习阅读

现在开始学习这个课程

Methali: Aanguae huanguliwa | | Habari za UN

Na sasa ni wasaa wa kujifunza Kiswahili. Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Aanguae huanguliwa.”

Aanguae huanguliwa. Ni methali iliyo na maana ya msingi kuwa, kuna wanyama ambao hutaga mayai. Mayai haya baadaye huanguliwa baada ya muda fulani wa kutunzwa na kupashwa joto na aliyeyataga. Huyu naye aliyeyataga naye katagwa na kuanguliwa. Ndiyo maana anataga na kuangua. Asingalifanywa na kuanguliwa hangalikuwepo. Inatufunza [methali] kwamba hakuna kinachotokana na ombwe tupu. Kila kitu kina asili yake. Hata kama mtu ana sifa gani, ziwe njema au mbovu, amezaliwa naye atazaa wake pia. Kwamba anayeonekana bora sana ameandaliwa vyema. Tusidharau asili yetu hata kidogo.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE