×

我们使用 cookie 帮助改善 LingQ。通过浏览本网站,表示你同意我们的 cookie 政策.

African Story Book Project, 02 Kuhesabu wanyama – 阅读文本

African Story Book Project, 02 Kuhesabu wanyama

初级1 斯瓦希里语 课程,练习阅读

现在开始学习这个课程

02 Kuhesabu wanyama

Tembo mmoja anakwenda kunywa maji.

Twiga wawili wanaenda kunywa maji.

Nyati watatu na ndege wanne nao wanaenda kunywa maji.

Swala watano na ngiri sita wanatembea kuelekea kwenye maji.

Punda milia saba wanakimbia kuelekea kwenye maji.

Vyura wanane na samaki tisa wanaogelea kwenye maji.

Simba mmoja anaunguruma. Naye anataka kunywa maji. Nani anamwogopa simba?

Tembo mmoja anakunywa maji na simba.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE