×

Vi använder kakor för att göra LingQ bättre. Genom att besöka sajten, godkänner du vår cookie policy.

image

Asili ya Afrika, Wangari Maathai: Mwanaharakati asiyeogopa - YouTube

Wangari Maathai: Mwanaharakati asiyeogopa - YouTube

Kutana na Wangari Maathai, mwanabiolojia, aliyekwenda kutembelea kijiji alikozaliwa miaka ya elfu moja tisa mia sabini (1970), na kuwakuta wanawake wakilalamikia uhaba wa kuni na maji ya kupikia. Alikumbuka utotoni mwake wakati vilima vilipokuwa vimefunikwa na miti na michirizi ya maji ikitiririka. Lakini miti hiyo baadaye ilikatwa, na badala yake kupandishwa mashamba ya chai na kahawa. Mfumo wa ekolojia ukaharibika. Wangari Maathai akapanga mpango, wa kupandisha miti na kuzuia mmomonyoko wa ardhi pamoja na michirizi ya maji kukauka. Kurejesha mazingira mazuri ya maeneo ya milimani kulifaidisha nchi nzima.

Wenzake kutoka kamati ya taifa ya wanawake wa Kenya walimuunga mkono. Na pamoja wakaanzisha Vuguvugu la Ukanda wa Kijani. Watu wenye vyeo pia waliunga mkono vuguvugu hilo la kupanda miti. Mwaka elfu moja, tisa mia tisini na nane (1998), msitu ulio katikati ya jiji la Nairobi uliteketezwa kabisa. Wangari Maathai alikasirishwa sana na hilo. Vuguvugu lake la Ukanda wa Kijani liligundua ujenzi ulioamrishwa na Rais Moi katikati ya msitu wa Karura. Kwa miezi kadhaa wakaanza kampeni ya kuhamasisha umma.

Makundi mengine yakaunga mkono lakini Moi na washirika wake hawakubabaishwa. Uvutano ukaanza na hata Wangari akarushiwa jiwe. Na mwa Agosti elfu moja tisa mia tisini na tisa (1999), Rais Moi alikubali kushindwa. Ujenzi ukasitishwa na vuguvugu la Maathai likaahidi kuukuza tena msitu huo.

Kwa Wangari Maathai kupanda miti ni kuhakikisha njia za kujipatia riziki. Mwaka elfu mbili na nne (2004) alipewa Tuzo ya Amani ya Nobeli. Mwaka elfu mbili na kumi na moja (2011) dunia nzima ilihuzunishwa na kifo chake. Na Vuguvugu la Ukanda wa Kijani likapata hadhi ya kimataifa.

Wangari Maathai: Mwanaharakati asiyeogopa - YouTube Wangari Maathai: Die furchtlose Aktivistin – YouTube Wangari Maathai: The Fearless Activist - YouTube Wangari Maathai: La activista intrépida - YouTube Wangari Maathai: The Fearless Activist - YouTube Wangari Maathai : l'activiste intrépide - YouTube Wangari Maathai: nieustraszona aktywistka – YouTube Wangari Maathai: a ativista destemida - YouTube Wangari Maathai:无所畏惧的活动家 - YouTube

Kutana na Wangari Maathai, mwanabiolojia, aliyekwenda kutembelea kijiji alikozaliwa miaka ya elfu moja tisa mia sabini (1970), na kuwakuta wanawake wakilalamikia uhaba wa kuni na maji ya kupikia. Meet Wangari Maathai, a biologist, who went to visit the village where he was born in the 1970s, and found women complaining about the lack of firewood and water for cooking. Alikumbuka utotoni mwake wakati vilima vilipokuwa vimefunikwa na miti na michirizi ya maji ikitiririka. He remembered his childhood when the hills were covered with trees and streams of water flowed. Lakini miti hiyo baadaye ilikatwa, na badala yake kupandishwa mashamba ya chai na kahawa. But the trees were later cut down, and replaced by tea and coffee plantations. Mfumo wa ekolojia ukaharibika. The ecological system was damaged. Wangari Maathai akapanga mpango, wa kupandisha miti na kuzuia mmomonyoko wa ardhi pamoja na michirizi ya maji kukauka. Wangari Maathai planned a plan to plant trees and prevent soil erosion and water streams to dry up. Kurejesha mazingira mazuri ya maeneo ya milimani kulifaidisha nchi nzima.