Uamuzi https://storybookscanada.ca/images/0027/02.jpg" alt="A crowd of people standing around a water tap."/> Kijiji changu kilikuwa na matatizo mengi. Tulipanga foleni ndefu tukisubiri kuchota maji kutoka mfereji mmoja. https://storybookscanada.ca/images/0027/03.jpg" alt="A line of people waiting for food donations."/> Tulisubiri kupokea msaada wa chakula. https://storybookscanada.ca/images/0027/04.jpg" alt="A woman locking her front door."/> Tulifunga nyumba zetu mapema kwasababu ya wizi. https://storybookscanada.ca/images/0027/05.jpg" alt="A man and woman standing next to a boy outside a school."/> Watoto wengi waliacha shule. https://storybookscanada.ca/images/0027/06.jpg" alt="Two girls dressed as maids walking through a village."/> Wasichana wadogo walifanya kazi za nyumbani kwenye vijiji vingine. https://storybookscanada.ca/images/0027/07.jpg" alt="Boys roaming around a village and a woman carrying shopping on her head."/> Wavulana wadogo waliranda randa kijijini na wengine walifanya kazi kwenye mashamba ya watu. https://storybookscanada.ca/images/0027/08.jpg" alt="Gusts of wind blowing waste paper onto trees."/> Upepo ulipovuma, ulipeperusha karatasi chafu na kuzifikisha mitini na uani. https://storybookscanada.ca/images/0027/09.jpg" alt="A boy sitting holding his injured foot."/> Watu walikatwa na vipande vya chupa vilivyotupwa ovyo ovyo. https://storybookscanada.ca/images/0027/10.jpg" alt="People standing around a water tap."/> Halafu siku moja, mfereji wa maji ulikauka na mitungi yetu ikawa mitupu. https://storybookscanada.ca/images/0027/11.jpg" alt="A man standing outside a house with two children talking with a woman."/> Baba yangu alitembea nyumba hadi nyumba akiwaomba watu kuhudhuria mkutano wa kijiji. https://storybookscanada.ca/images/0027/12.jpg" alt="People sitting under a big tree listening to a man speaking."/> Watu walikusanyika chini ya mti mkubwa na kusikiliza. https://storybookscanada.ca/images/0027/13.jpg" alt="A man speaking to a crowd of people sitting under a tree."/> Baba yangu alisimama na kusema, “Tunahitaji kusaidiana kutatua matatizo yetu.” https://storybookscanada.ca/images/0027/14.jpg" alt="A boy sitting on a tree trunk raising his hand."/> Juma, mtoto wa miaka minane aliyekuwa amekaa kwenye tawi la mti, alisema kwa sauti, “Naweza kusaidia na usafi.” https://storybookscanada.ca/images/0027/15.jpg" alt="A woman suggesting women join her to grow food."/> Mwanamke mmoja alisema, “Sisi wanawake tunaweza kuungana na kulima.” https://storybookscanada.ca/images/0027/16.jpg" alt="A man suggesting men help to dig a well."/> Mwanamume mwingine alisimama na kusema, “Wanaume watachimba kisima cha maji.” https://storybookscanada.ca/images/0027/17.jpg" alt="A crowd of people standing together smiling."/> Sote tulisema kwa sauti moja, “Lazima tubadilishe maisha yetu.” Tangu siku hiyo, tulifanya kazi pamoja kutatua shida zetu.