Tom muuza ndizi https://storybookscanada.ca/images/0296/02.jpg" alt="A man carrying a tray of bananas on his head."/> Tom anabeba tenga la ndizi zilizoiva. https://storybookscanada.ca/images/0296/03.jpg" alt="A man walking with a tray of bananas on his head."/> Tom anaenda sokoni kuuza ndizi. https://storybookscanada.ca/images/0296/04.jpg" alt="People buying fruit at a market."/> Sokoni watu wananunua matunda. https://storybookscanada.ca/images/0296/05.jpg" alt="A man standing at a banana stall."/> Lakini hakuna anayenunua ndizi za Tom. Wanapenda kununua matunda kutoka kwa akina mama. https://storybookscanada.ca/images/0296/06.jpg" alt="A man sitting at a banana stall."/> “Kwenye jamii yetu, ni wanawake pekee ndio wanaouza matunda,” watu wanasema. “Ni mwanamume wa aina gani huyu?” watu wanahoji. https://storybookscanada.ca/images/0296/07.jpg" alt="A man standing at a banana stall and people walking towards him."/> Lakini Tom hakati tamaa. Anaita, “Nunua ndizi zangu! Nunueni ndizi zangu tamu zilizoiva!” https://storybookscanada.ca/images/0296/08.jpg" alt="A woman holding a bunch of bananas and a man standing at a banana stall passing her bananas."/> Mwanamke mmoja anachukua kichane cha ndizi kutoka kwenye tenga. Anaziangalia ndizi kwa umakini. https://storybookscanada.ca/images/0296/09.jpg" alt="A woman holding up a bunch or bananas in a market."/> Mwanamke ananunua ndizi. https://storybookscanada.ca/images/0296/10.jpg" alt="A man standing at a banana stall and people walking towards him."/> Watu wengine wanakuja kwenye kichanja. Wananunua ndizi za Tom na kuzila. https://storybookscanada.ca/images/0296/11.jpg" alt="A man standing with an empty tray at a market stall and people eating bananas."/> Mara, tenga linakuwa tupu. Tom anahesabu pesa alizopata. https://storybookscanada.ca/images/0296/12.jpg" alt="A man buying items from a market stall and putting them in a tray."/> Tom ananunua sabuni, sukari, na mkate. Anaweka vitu kwenye tenga lake. https://storybookscanada.ca/images/0296/13.jpg" alt="A man carrying a tray on his head."/> Tom anajitwisha tenga kichwani na kwenda nyumbani.