×

우리는 LingQ를 개선하기 위해서 쿠키를 사용합니다. 사이트를 방문함으로써 당신은 동의합니다 쿠키 정책.

Storybooks Canada, Khalai azungumza na mimea – 읽을 텍스트

Storybooks Canada, Khalai azungumza na mimea

초급 1 읽기를 연습하는 스와힐리어 수업

지금 본 레슨 학습 시작

Khalai azungumza na mimea

https://storybookscanada.ca/images/0089/02.jpg" alt="A girl in a field waving."/>

Khalai ni msichana mwenye umri wa miaka saba. Jina lake lina maana ya ‘aliye mzuri' katika lugha yake ya Lubukusu.

https://storybookscanada.ca/images/0089/03.jpg" alt="A girl talking to an orange tree."/>

Khalai anaamka na kuongea na mmea mchanga wa Mchungwa, “Tafadhali mti wa Mchungwa, kua mkubwa uzae machungwa mengi mabivu.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/04.jpg" alt="A girl kneeling on the ground talking to grass."/>

Khalai anaenda shuleni na njiani anaongea na Nyasi, “Tafadhali Nyasi, kua kijani zaidi na zaidi na wala usikauke.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/05.jpg" alt="A girl looking at wild flowers."/>

Khalai anayapita Maua ya mwituni na kusema, “Tafadhali Maua, endelea kunawiri ili niweze kukuweka kwenye nywele zangu.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/06.jpg" alt="A girl next to a tree in a school playground."/>

Akiwa shuleni, Khalai anazunguumza na Mti ulioko katikati ya shule, “Tafadhali Mti, toa matawi makubwa ili tusome chini ya kivuli chako.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/07.jpg" alt="A girl talking to a hedge outside a school."/>

Khalai anazunguumza na ua unaoizingira shule yake, “Tafadhali ua, kuwa mwenye nguvu ili uzuie shule yetu kutokana na watu wabaya.”

https://storybookscanada.ca/images/0089/08.jpg" alt="A girl next to an orange tree."/>

Anaporudi nyumbani alasiri, Khalai anautembelea mti wa Mchungwa kuangalia kama machungwa yameiva.

https://storybookscanada.ca/images/0089/09.jpg" alt="A girl next to an orange tree."/>

“Machungwa bado mabichi,” Khalai anashusha pumzi. “Nitakuona kesho, we mti wa machungwa. Labda utanipa chungwa bivu wakati huo.”

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE