×

우리는 LingQ를 개선하기 위해서 쿠키를 사용합니다. 사이트를 방문함으로써 당신은 동의합니다 쿠키 정책.

Habari za UN, Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "NDUI" | |... – 읽을 텍스트

Habari za UN, Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "NDUI" | | Habari za UN

중급 2 읽기를 연습하는 스와힐리어 수업

지금 본 레슨 학습 시작

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "NDUI" | | Habari za UN

Na tugeukie katika kujifunza lugha adhimu ya Kiswahili na leo tunapata ufafanuzi wa neno "NDUI" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.

Ndui ni ugonjwa ambao sasa hivi watu wengi hawaufahamu. Huu ni ugonjwa kama vile tetekuwanga, ambao unaenezwa na virusi vinavyoshambulia mwili aghalabu huwacha madoadoa meusi kwenye ngozi baada ya kupona. Ni aina ya upele ambao unampata mtu na ugonjwa huo unaambukizwa na virusi. Na huu ni ugonjwa ambao ulikuweko sana miaka ya nyuma. Sasa hivi ni nadra kutokana na chanjo mbalimbali ambazo watu wanazipata. Lakini pia inaweza kutokana na mazingira na ukomavu wa sayansi na teknolojia katika kuthibiti virusi hivi.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE