×

우리는 LingQ를 개선하기 위해서 쿠키를 사용합니다. 사이트를 방문함으로써 당신은 동의합니다 쿠키 정책.

Habari za UN, Jifunze kiswahili: Je, wajua maana ya neno ... – 읽을 텍스트

Habari za UN, Jifunze kiswahili: Je, wajua maana ya neno "KUYEYESA"? | | Habari za UN

중급 2 읽기를 연습하는 스와힐리어 수업

지금 본 레슨 학습 시작

Jifunze kiswahili: Je, wajua maana ya neno "KUYEYESA"? | | Habari za UN

Na sasa ni wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili. Leo tunafafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA". Na mtaalam wetu Onni Sigalla. Huyu ni Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.

Mara nyingi tunafanya usaidizi kwa wenzetu na hasa ambao wamepatwa na maradhi kwa muda mrefu, wameishiwa nguvu au kwa mtu ambaye umri wake umemsogea sana na anahitaji usaidizi. Kitendo hicho si usaidizi kama ambavyo tunasema ila tunaweza tukasema ni uyeyesaji. Yaani, unayeyesa, au unayeyeswa, au unayeyesesha mtu ambaye aghalabu; ni mgonjwa ili aweze kutembea au kukua na nguvu tena ili aweze kutembea. Kwa hiyo, mtu unapomsaidia, mtu aweze kutembea, aweze kujongea mahali fulani, basi unakuwa unamyeyesa na kama ni wewe mwenyewe basi unayeyesewa na kadhalika.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE