×

우리는 LingQ를 개선하기 위해서 쿠키를 사용합니다. 사이트를 방문함으로써 당신은 동의합니다 쿠키 정책.

LingQ Mini Stories, 7- Ninafanya Kazi Ofisini – 읽을 텍스트

LingQ Mini Stories, 7- Ninafanya Kazi Ofisini

초급 1 읽기를 연습하는 스와힐리어 수업

지금 본 레슨 학습 시작

Joseph anafanya kazi ofisini.

Ametingwa sana na kazi kila siku.

Huwa ana vikao vingi na wateja wake.

Joseph huwa hapendi vikao hivi.

Huwa anafikiri kwamba vinaboa sana.

Baadhi ya wateja ni wakarimu kwa Joseph.

Ila, baadhi ya wateja sio wakarimu.

Joseph huwa anachukua mapumziko marefu muda wa chakula cha mchana.

Anaweza kwenda nyumbani saa kumi na moja.

Huwa anasubiri kila siku saa kumi na moja ifike.

Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na Joseph.

Ninafanya kazi ofisini.

Huwa nimetingwa sana na kazi kila siku.

Huwa nina vikao vingi na wateja wangu.

Sivipendi vikao hivi.

Ninafikiria kwamba vinaboa sana.

Baadhi ya wateja ni wakarimu kwangu.

Ila, baadhi ya wateja sio wakarimu.

Huwa ninachukua mapumziko marefu muda wa chakula cha mchana.

Ninaweza kwenda nyumbani saa kumi na moja jioni.

Huwa ninasubiri kila siku saa kumi na moja ifike.

Maswali.

1) Joseph anafanya kazi ofisini. Je, Joseph anafanya kazi shuleni? Hapana, Joseph anafanya kazi ofisini.

2) Joseph huwa ametingwa sana na kazi kila siku. Je, Joseph ametingwa sana na kazi? Ndiyo, Joseph ametingwa sana na kazi kila siku.

3) Joseph huwa ana vikao vingi na wateja wake. Je Joseph huwa ana vikao vichache? Hapana, Joseph huwa ana vikao vingi na wateja wake.

4) Joseph huwa anafikiri kwamba vikao vinaboa. Je, Joseph anafikiri vikao vinaboa? Ndiyo, Joseph huwa anafikiri vikao vinaboa.

5) Baadhi ya wateja ni wakarimu. Je, wateja wote ni wakarimu? Hapana, baadhi ya wateja ni wakarimu.

6) Joseph huwa anachukua mapumziko marefu muda wa chakula cha mchana. Je, Joseph huwa anachukua mapumziko mafupi muda wa chakula cha mchana? Hapana, huwa hachukui mapumziko mafupi. Huwa anachukua mapumziko marefu muda wa chakula cha mchana.

7) Joseph anaweza kwenda nyumbani saa kumi na moja jioni. Je, Joseph anaweza kwenda nyumbani saa kumi? Hapana, anaweza kwenda nyumbani saa kumi na moja.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE