×

우리는 LingQ를 개선하기 위해서 쿠키를 사용합니다. 사이트를 방문함으로써 당신은 동의합니다 쿠키 정책.

LingQ Mini Stories, 4- Ni Mwanafunzi Mzuri – 읽을 텍스트

LingQ Mini Stories, 4- Ni Mwanafunzi Mzuri

초급 1 읽기를 연습하는 스와힐리어 수업

지금 본 레슨 학습 시작

Binti yangu huwa anakwenda shule kila siku.

Huwa anapenda shule sana.

Ni mwanafunzi mzuri shuleni.

Walimu wanampenda binti yangu sana.

Binti yangu pia ana marafiki wengi.

Rafiki yake wa karibu ni Mariam.

Mariam huwa anapenda hisabati na sayansi.

Binti yangu huwa anapenda Kiingereza na historia.

Huwa wanasaidiana na kazi zao za nyumbani.

Wanasoma kwa bidii na wanafanya vizuri shuleni.

Hii ni hadithi hiyo, ikisimuliwa na binti huyo.

Huwa ninakwenda shule kila siku.

Ninapenda shule sana

Mimi ni mwanafunzi mzuri shuleni.

Walimu wangu wananipenda sana.

Pia nina marafiki wengi.

Rafiki yangu wa karibu ni Mariam.

Huwa anapenda hesabu na sayansi.

Mimi ninapenda Kiingereza na historia.

Huwa tunasaidiana na kazi zetu za nyumbani.

Tunasoma kwa bidii na tunafanya vizuri shuleni.

Maswali:

1) Binti huyo huwa anakwenda shuleni kila siku. Je, binti huyo huwa anaenda shuleni kila siku? Ndiyo, huwa anaenda shule kila siku.

2) Binti huyo huwa anapenda shule. Je, Binti huyo huwa anapenda shule? Ndiyo, huwa anapenda shule.

3) Binti huyo ni mwanafunzi mzuri. Je, binti huyu ni mwanafunzi mbaya? Hapana, binti huyo sio mwanafunzi mbaya. Ni mwanafunzi mzuri.

4) Walimu wanampenda binti huyo. Je, walimu wanampenda binti huyo? Ndiyo, walimu wanampenda.

5) Rafiki yake wa karibu anaitwa Mariam. Je, rafiki yake wa karibu anaitwa Anna? Hapana, rafiki yake wa karibu anaitwa Mariam.

6) Mariam huwa anapenda hisabati na sayansi. Je, Mariam huwa anapenda Kiingeleza na historia? Hapana, huwa anapenda hisabati na sayansi.

7) Binti huyo na Mariam wanafanya vizuri shuleni. Je, binti huyo anafanya vizuri shuleni? Ndiyo, binti huyo na Mariam wanafanya vizuri shuleni.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE