×

We use cookies to help make LingQ better. By visiting the site, you agree to our cookie policy.

image

Swahili dialogue - Nchi ya Mwujiza, Nchi ya Mwujiza

Nchi ya Mwujiza

017 Mawe Moja, Kendu Bay Februari 20, 2016

Hujambo mpendwa binamu! Ninatumai hujambo.

Nisamehe kwa kuchelewa kujibu maswali yako kuhusu safari yangu ya kuvutia ya Kenya.

Unajua kwamba nimekuwa nje ya bara letu kwa muda.

Safari yangu ilikuwa ya siku saba. Nilisafiri na ndege ya Kenya Airways kutoka Ulaya ya Kati.

Nilifurahi sana kutembelea bara la Afrika kwa mara ya kwanza.

Siku ya kwanza ya safari yetu tulitembelea karibu katikati ya mji wa Kisumu kufurahia hali ya hewa nzuri.

Ilikuwa ni siku ya mapumziko.

Siku ya pili, mwongozo alituchukua vivutio mbalimbali vya utalii na kisha ununuzi.

Niamini, unaweza kupata zawadi ya bei nafuu nchini Kenya.

Sehemu ya kuvutia ya safari yetu ilikuwa kwenda Nairobi kupitia mabasi ambao ulifanyika siku ya tatu.

Sanaa ya mwamba katika barabara na vijiji vya jirani ni kuvutia sana.

Wakati huko, tulitembelea Makumbusho Maarufu ya Taifa ya Nairobi na kisha tukaenda bustani ya mimea.

Pengine unajua kwamba kuna ndenge nyingi za changamfu na vipepeo nchini Kenya.

Tulitumia siku nne ya mwisho ya safari yetu kwa kujifurahisha katika Kisiwa ya Lamu na mji wake wa kale.

Siku ya mwisho katika saa za alasiri tulirudi kwa mji mkuu, Nairobi nakujitaharisha kuondoka wakati wa usiku.

Nataka kwenda huko tena pengine mwaka ujao.

Nashangaa kama ungependa kuandamana nami kwa nchi ya mwujiza ya Kenya.

Kwaheri kwa sasa, ninamatumaini ya kusikia kutoka kwako kuhusu safari yako Ulaya.

Asante sana, Kanyaga.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE