×

We use cookies to help make LingQ better. By visiting the site, you agree to our cookie policy.

image

Habari za UN, TANBAT 6, Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wapokea pongezi kutoka JWTZ na MINUSCA | | Habari za UN

TANBAT 6, Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wapokea pongezi kutoka JWTZ na MINUSCA | | Habari za UN

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 6 cha kutoka Tanzania TANBAT 06 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wamepokea ugeni na salamu kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia ujumbe uliongozwa na Brigedia Jenerali George Mwita Itang'are aliyewakilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kutokana na sifa nzuri anazozipokea kutoka MINUSCA kuhusu kikosi hicho. Kutoka mjini Berbérati mkoani Mambéré-Kadéï, Afisa Habari wa TANBAT 06 Kapteni Mwijage Inyoma ameshiriki mapokezi ya ugeni huo, na hii ni taarifa yake.

Kwanza ni gwaride la ukaguzi…na kisha baadaye ukumbini ni nyimbo za morali. Brigedia Jenerali Itangare katika ziara hii aliyoambatana na Brigedia Jenerali Robert William Mtafungwa ambaye ni Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa akizungumza na maafisa na askari walinda amani baada ya ziara yake ya kutembea kikosi hicho amesema kuwa lengo la ziara ya ujumbe huo ni kuangalia utayari wa kikosi lakini pia kuwapongeza kwa kazi nzuri na utayari pale wanapopewa jukumu.

Aidha Brigedia Jenerali Itang'are amewataka walinda amani hao kuzingatia maadili ili wasiuchafue Umoja wa Mataifa, Jeshi la Tanzania na taifa lao.

Kwa upande wake Mkuu wa TANBAT 06 Luteni Kanali Amini Stephen Mshana ameshukuru Jeshi la Tanzania kufanya ziara ya kutembelea kikosi hicho nchini CAR lakini pia akawakumbusha askari yaliyozungumzwa amehahidi kuendeleza mafanikio waliyoyaona ikiwemo kutekeleza maelekezo ambayo wameyapokea.

TANBAT 6, Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wapokea pongezi kutoka JWTZ na MINUSCA  | | Habari za UN TANBAT 6, UN-Friedenstruppen aus Tansania erhalten Glückwünsche von JWTZ und MINUSCA | UN-Nachrichten TANBAT 6, UN peacekeepers from Tanzania receive congratulations from JWTZ and MINUSCA | UN news TANBAT 6, las fuerzas de paz de la ONU de Tanzania reciben felicitaciones de JWTZ y MINUSCA | noticias de la ONU TANBAT 6, forças de paz da ONU da Tanzânia recebem parabéns da JWTZ e da MINUSCA | notícias da ONU TANBAT 6,来自坦桑尼亚的联合国维和人员受到JWTZ和中非稳定团的祝贺|联合国新闻