×

We use cookies to help make LingQ better. By visiting the site, you agree to our cookie policy.

image

Habari za UN, Kiliniki za UNICEF zinazotembea msaada kwa waathirika wa kimbunga Freddy nchini Malawi | | Habari za UN

Kiliniki za UNICEF zinazotembea msaada kwa waathirika wa kimbunga Freddy nchini Malawi | | Habari za UN

Wananchi wa Malawi walioathirika na Kimbunga Freddy wamepongeza mbinu ya kutumia kilniki za kuhama kwa njia ya magari iliyotumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwahudumia wanawake na watoto nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kilicholipiga eneo hilo takribani miezi mwili iliyopita.

Anold Kayanda amefuatilia na kutuandalia taarifa hii.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) linasema kimbunga Freddy kilichotokea kati ya Februari 5 na Machi 14 kiliwaacha watoto wa Malawi milioni 2.9 hatarini na katika uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu.

Na katika msingi huo bado UNICEF inawaomba wahisani duniani kote kuichangia dola za Marekani milioni 52.4 kupitia ombi la Hatua ya Kibinadamu kwa ajili ya kufanikisha kutoa msaada wa kuokoa maisha ya watoto na wanawake nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na wale walioathiriwa na Kimbunga Freddy hicho.

Hata hivyo UNICEF katika hali hiyo hiyo ya uhaba wa ufadhili bado ilifanikiwa kutoa msaada kwa watu walioalazimika kuishi kwenye makambi baada ya kimbunga hicho. Mary Kwatani ni mmoja wao, “Nilikuja kambini kwa sababu nilipoteza nyumba yangu kutokana na mafuriko. Nilikuja hapa kutafuta makazi kwa sababu afya ya watoto wangu ilikuwa mbaya kutokana na lishe duni.”

Kwa haraka UNICEF ilichukua hatua ikaleta kiliniki za kwenye magari ili kuleta huduma tiba kwa ajili ya, wajawazito na wanaonyesha na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Mary Kwatani ni mnufaika anasema, "Kiliniki hizi zinazotembea zimekuwa msaada kwangu kwa sababu nilikuwa nasafiri umbali mrefu kufika hospitalini lakini sasa wahudumu wa afya wanaweza kutufikia kupitia kiliniki zinazohama."

Kimbunga Freddy ambacho kilizipiga nchi kadhaa kusini mwa Afrika, kwa Malawi kiliathiri moja kwa moja wilaya 15 zilizopo kusini mwa nchi ya Malawi na kuathiri maisha ya watu na makazi.

Kiliniki za UNICEF zinazotembea msaada kwa waathirika wa kimbunga Freddy nchini Malawi | | Habari za UN UNICEF-Kliniken, die den Opfern des Zyklons Freddy in Malawi helfen | | UN-Nachrichten UNICEF clinics that help the victims of Cyclone Freddy in Malawi | | UN news Clínicas de UNICEF que ayudan a las víctimas del ciclón Freddy en Malawi | | noticias de la ONU Cliniques de l'UNICEF qui aident les victimes du cyclone Freddy au Malawi | | Actualités de l'ONU UNICEF-klinieken die de slachtoffers van cycloon Freddy in Malawi helpen | | VN-nieuws clínicas da UNICEF que ajudam as vítimas do ciclone Freddy no Malawi | | notícias da ONU клиники ЮНИСЕФ, которые помогают жертвам циклона Фредди в Малави | | Новости ООН 聯合國兒童基金會診所為馬拉維颶風弗雷迪的受害者提供幫助|聯合國新聞