×

We use cookies to help make LingQ better. By visiting the site, you agree to our cookie policy.


image

Habari za UN, Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama" | | Habari za UN

Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama" | | Habari za UN

Na sasa kama nilivyokuahidi, ni wasaa wa kujifunza Kiswahili na leo hii nampisha Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) nchini Tanzania. Si mwingine bali ni Dkt. Mwanahija Ally Juma akituchambulia methali: Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama!

Mama ni mama hata kama ni rikwama. Mama ni mzazi mwanamke ambaye mara nyingi anachukua nafasi kubwa katika kumleta au kumzaa mtoto. Na anachukua nafasi kubwa katika kumhudumia mtoto tokea yuko tumboni hadi anazaliwa, hadi kukua kwake.

Na rikwama ni kifaa ambacho kinatumika kubebea mizigo. Kwa hiyo, hata kama mama anafanya kazi nyingi, ana nafasi kubwa katika malezi, ana shughuli nyingi za kumhudumikia mtoto, anabeba mazuri na mabaya, shida na dhiki, lakini bado atakuwa ni mama, na ana umuhimu sana katika familia na katika jamii. Kwa hiyo, mama ni mama hata kama ni rikwama.

Hata kama mama analazimika kufanya pilka nyingi, kubeba machungu, kubeba maovu, kubeba furaha, kubeba dhiki, kubeba shida, lakini bado ni mama na anastahili kutunzwa. Anastahili kupewa heshima. Kufikiriwa kwa mujibu wa uzito wake. Kwa kuwa ni rikwama anachukuliwa kama ni kitu ambacho kimetelekezwa kubeba vitu vizuri, vitu vichafu mbalimbali. Kazi yake ni kuzibeba tu lakini thamani yake ni ndogo. Ikimaliza kubeba inawekwa pembeni. Kwa hiyo mama ni mama. Bado anayo nafasi ya kuthaminiwa, ya kusaidiwa. Anayo nafasi ya kupewa umuhimu na uzito unaofaa hata kama ana shida nyingi ambazo zinamsibu na anajitwika na mazonge mengi kutokea uzazi, malezi, shida, matatizo, dhiki za watoto, na dhiki zake yeye bado zinamkabidhi. Lakini bado ni mama na anastahili heshima yote.

Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama" | | Habari za UN Kiswahili lernen: „Eine Mutter ist eine Mutter, auch wenn sie eine Rikwama ist“ | | UN-Nachrichten Learn Kiswahili: "A mother is a mother even if she is a Rikwama" | | UN news Aprende kiswahili: "Una madre es una madre aunque sea una Rikwama" | | noticias de la ONU Apprendre le Kiswahili : « Une mère est une mère même si elle est Rikwama » | | Actualités de l'ONU スワヒリ語を学ぶ: 「たとえリクワマであっても、母親は母親です」 | |国連ニュース Aprenda Kiswahili: "Uma mãe é uma mãe mesmo que seja uma Rikwama" | | notícias da ONU

Na sasa kama nilivyokuahidi, ni wasaa wa kujifunza Kiswahili na leo hii nampisha Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) nchini Tanzania. And now, as I promised you, it is time to learn Kiswahili and today I appoint the Executive Secretary of the Kiswahili Council of Zanzibar (BAKIZA) in Tanzania. Si mwingine bali ni Dkt. None other than Dr. Mwanahija Ally Juma akituchambulia methali: Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama! Pilgrim Ally Juma analyzing a proverb for us: A mother is a mother even if she is Rikwama!

Mama ni mama hata kama ni rikwama. A mother is a mother even if she is a mother. Mama ni mzazi mwanamke ambaye mara nyingi anachukua nafasi kubwa katika kumleta au kumzaa mtoto. A mother is a female parent who often takes a big role in bringing or giving birth to a child. Na anachukua nafasi kubwa katika kumhudumia mtoto tokea yuko tumboni hadi anazaliwa, hadi kukua kwake. And he takes a big role in caring for the child from the time he is in the womb until he is born, until he grows up.

Na rikwama ni kifaa ambacho kinatumika kubebea mizigo. And a cart is a device that is used to carry goods. Kwa hiyo, hata kama mama anafanya kazi nyingi, ana nafasi kubwa katika malezi, ana shughuli nyingi za kumhudumikia mtoto, anabeba mazuri na mabaya, shida na dhiki, lakini bado atakuwa ni mama, na ana umuhimu sana katika familia na katika jamii. Therefore, even if a mother works a lot, has a big role in upbringing, has many activities to serve the child, carries the good and the bad, problems and stress, but she will still be a mother, and she is very important in the family and in the society. Kwa hiyo, mama ni mama hata kama ni rikwama.

Hata kama mama analazimika kufanya pilka nyingi, kubeba machungu, kubeba maovu, kubeba furaha, kubeba dhiki, kubeba shida, lakini bado ni mama na anastahili kutunzwa. Even if a mother has to do a lot of pilka, bear pains, bear evils, bear happiness, bear stress, bear problems, but she is still a mother and deserves to be taken care of. Anastahili kupewa heshima. He deserves respect. Kufikiriwa kwa mujibu wa uzito wake. Considered according to its weight. Kwa kuwa ni rikwama anachukuliwa kama ni kitu ambacho kimetelekezwa kubeba vitu vizuri, vitu vichafu mbalimbali. Kazi yake ni kuzibeba tu lakini thamani yake ni ndogo. Since it is a cart, it is treated as something that has been abandoned to carry good things, various dirty things. His job is just to carry them but his value is small. Ikimaliza kubeba inawekwa pembeni. When finished carrying it is put aside. Kwa hiyo mama ni mama. So a mother is a mother. Bado anayo nafasi ya kuthaminiwa, ya kusaidiwa. He still has a chance to be appreciated, to be helped. Anayo nafasi ya kupewa umuhimu na uzito unaofaa hata kama ana shida nyingi ambazo zinamsibu na anajitwika na mazonge mengi kutokea uzazi, malezi, shida, matatizo, dhiki za watoto, na dhiki zake yeye bado zinamkabidhi. He has the opportunity to be given importance and appropriate weight even if he has many problems that are affecting him and he is burdened with many conversations arising from parenting, upbringing, problems, problems, children's distress, and his own distress is still entrusted to him. Lakini bado ni mama na anastahili heshima yote. But she is still a mother and deserves all the respect.