Agnes alihitaji kwenda kazini.
Alikuwa anajaribu kuwasha gari lake.
Lakini kulikuwa na baridi sana nje, hivyo gari lake likawa haliwaki.
Kwanza akatazama ratiba za basi.
Angechelewa kama angechukua basi.
Kisha akatazama ratiba za treni.
Treni zilikuwa zinafika ndani ya muda.
Akaamua kuchukua treni kwenda kazini.
Alikuwa akitarajia hatachelewa kazini.
Hii ni hadithi hiyo ikisimuliwa na Agnes.
Nilihitaji kwenda kazini.
Nilijaribu kuwasha gari langu.
Lakini kulikuwa na baridi sana nje.
Hivyo gari langu halikuwaka.
Kwanza nilitazama ratiba za basi.
Ningechelewa kama nitachukua basi.
Kisha nikatazama ratiba za treni.
Treni zilikuwa zinafika ndani ya muda.
Nikaamua kuchukua treni kwenda kazini.
Nilikuwa nikitarajia sitachelewa kazini.
Maswali.
1) Agnes anajaribu kwenda kazini. Je, Agnes alikuwa anajaribu kwenda kazini? Ndiyo, Agnes alikuwa anajaribu kwenda kazini.
2) Kulikuwa na baridi nje. Je, kulikuwa na joto nje? Hapana, hakukuwa na joto nje. Kulikuwa na baridi nje.
3) Gari la Agnes halikuwaka kwa sababu kulikuwa na baridi sana nje. Je, gari la Agnes liliwaka? Hapana, gari la Agnes halikuwaka kwa sababu kulikuwa na baridi sana nje.
4) Baada ya hapo, Agnes alitazama ratiba za basi. Je, Agnes alitazama ratiba za treni kwanza? Hapana, hakufanya hivyo. Agnes alitazama ratiba za basi kwanza.
5) Agnes angechelewa kama angechukua basi. Je, Agnes angefika ndani ya muda kama angechukua basi? Hapana, angechelewa kama angechukua basi.
6) Treni zilikuwa zinafika ndani ya muda. Je, treni zilikuwa zinachelewa? Hapana, treni zilikuwa hazichelewi. Zilikuwa zinafika ndani ya muda.
7) Agnes aliamua kuchukua treni kwenda kazini. Je, Agnes aliamua kuchukua basi kwenda kazini? Hapana, Agnes hakuamua kuchukua basi. Aliamua kuchukua treni kwenda kazini.
8) Agnes alitarajia hatachelewa kazini. Je, Agnes alitaka kuchelewa kazini? Hapana, hakutaka kuchelewa kazini. Alitarajia hatachelewa kazini.