×

Vi använder kakor för att göra LingQ bättre. Genom att besöka sajten, godkänner du vår cookie-policy.

image

Habari za UN, WHO: Nchi ziache kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku | | Habari za UN

WHO: Nchi ziache kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku | | Habari za UN

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezisihi nchi kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na badala yake kuelekeza usaidizi wao kwenye mazao endelevu yatakayo wanufaisha mamilioni ya watu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

Katika kuelekea siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani itakayoadhimishwa Mei 31 WHO inasema , watu milioni 300 ulimwenguni wanakabiliwa na uhaba wa chakula wakati huo huo zaidi ya hekta milioni 3 katika nchi 120 zinatumika kulima tumbaku, hata katika zile nchi zenye tatizo la njaa.

WHO katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo huko Geneva Uswisi imeeleza kuwa kwa kuchagua kulima mazao ya chakula badala ya tumbaku inamaanisha jamii inatoa kipaumbele kwenye afya, kulinda baianowai na kuimarisha uhakika wa chakula.

Akizungumzia athari za tumbaku, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “tumbaku imesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 8 kwa mwaka, na bado serikali duniani kote zinatumia mamilioni ya kuwasaidia wakulima wa zao hilo.”

Ripoti mpya iliyotolewa na WHO kuelekea siku ya kupinga matumizi ya tumbaku iitwayo “Lima chakula sio tumbaku” imeeleza madhara ya kulima tumbaku na faida ambazo wakulima, jamii, uchumi, mazingira na dunia kwa ujumla itapata iwapo itahamia kwenye ukulima wa mazao mengine.

Ripoti hiyo pia inafichua tasnia ya tumbaku kuwa inawaingiza wakulima katika changamoto mbalimbali ikiwemo mzunguko mbaya wa madeni, wakulima kupata magonjwa na watoto zaidi ya milioni 1 wametumbukia kwenye kilimo hicho na kukosa fursa ya kupata elimu.

Katika kuhakikisha wakulima wanasaidiwa kuhamia kwenye kilimo cha mazao ya chakula WHO kwa kushirikiana na mashirika mengine ya UN lile la Mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wanawasaidia wakulima 5000 nchini Kenya na Zambia kulima mazoa ya chakula endelevu badala ya tumbaku.

Katika juhudi hizo WHO kila mwaka katika siku ya Kutotumia tumbaku huwaenzi wale wanaoleta mabadiliko chanya katika udhibiti wa tumbaku na mwaka huu mmoja wa washindi wa Tuzo hizo, Bi. Sprina Robi Chacha, mkulima wa kike kutoka nchini Kenya ambaye anatambulika si tu kwa kuachana na kilimo cha tumbaku kuhamia kwenye maharagwe yenye protini nyingi, bali pia kutoa mafunzo kwa mamia ya wakulima wengine ili na wao waweze kutoka kwenye kilimo cha tumbaku na kujenga jamii yenye afya bora.

WHO: Nchi ziache kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku | | Habari za UN WER: Länder sollten aufhören, Tabakbauern zu subventionieren | UN-Nachrichten WHO: Countries should stop subsidizing tobacco farmers | UN news OMS: Los países deberían dejar de subsidiar a los productores de tabaco | noticias de la ONU OMS : Les pays devraient cesser de subventionner les producteurs de tabac | Actualités de l'ONU Oms: i paesi dovrebbero smettere di sovvenzionare i coltivatori di tabacco | Novità dell'ONU WHO:各国はタバコ農家への補助金をやめるべきだ|国連ニュース WHO: Kraje powinny zaprzestać dotowania rolników uprawiających tytoń | Wiadomości ONZ OMS: os países devem parar de subsidiar os produtores de tabaco | notícias da ONU DSÖ: Ülkeler tütün çiftçilerine verilen sübvansiyonu durdurmalı | BM haberleri

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezisihi nchi kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na badala yake kuelekeza usaidizi wao kwenye mazao endelevu yatakayo wanufaisha mamilioni ya watu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. Get more information from Leah Mushi.

Katika kuelekea siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani itakayoadhimishwa Mei 31 WHO inasema , watu milioni 300 ulimwenguni wanakabiliwa na uhaba wa chakula wakati huo huo zaidi ya hekta milioni 3 katika nchi 120 zinatumika kulima tumbaku, hata katika zile nchi zenye tatizo la njaa.

WHO katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo huko Geneva Uswisi imeeleza kuwa kwa kuchagua kulima mazao ya chakula badala ya tumbaku inamaanisha jamii inatoa kipaumbele kwenye afya, kulinda baianowai na kuimarisha uhakika wa chakula. WHO in their press release issued today in Geneva, Switzerland has explained that by choosing to grow food crops instead of tobacco, it means that society gives priority to health, protecting biodiversity and enhancing food security.

Akizungumzia athari za tumbaku, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “tumbaku imesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 8 kwa mwaka, na bado serikali duniani kote zinatumia mamilioni ya kuwasaidia wakulima wa zao hilo.” Speaking about the effects of tobacco, WHO Director General Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus said "tobacco has caused the deaths of more than 8 million people a year, and yet governments around the world are spending millions to help the farmers of that crop."

Ripoti mpya iliyotolewa na WHO kuelekea siku ya kupinga matumizi ya tumbaku iitwayo “Lima chakula sio tumbaku” imeeleza madhara ya kulima tumbaku na faida ambazo wakulima, jamii, uchumi, mazingira na dunia kwa ujumla itapata iwapo itahamia kwenye ukulima wa mazao mengine. A new report issued by WHO towards the day against tobacco use called "Grow food is not tobacco" has explained the effects of growing tobacco and the benefits that farmers, society, the economy, the environment and the world in general will get if they move to the cultivation of other crops.