×

Vi använder kakor för att göra LingQ bättre. Genom att besöka sajten, godkänner du vår cookie-policy.


image

Habari za UN, WHO imetoa onyo kwamba matumizi ya vikoleza utamu visivyo sukari hayapunguzi uzito | | Habari za UN

WHO imetoa onyo kwamba matumizi ya vikoleza utamu visivyo sukari hayapunguzi uzito | | Habari za UN

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, hii leo limetoa mwongozo unaoshauri watu wasitumie vikoleza utamu visivyo sukari halisia (NSS) kwa lengo la kupunguza uzito na kuepusha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.

Assumpta Massoi anafafanua zaidi.

Taarifa ya WHO iliyotolewa leo Geneva, Uswisi inasema mwongozo huo unafuatia mapitio ya ushahidi unaodokeza kwamba kutumia sukari isiyo halisia kwa ajili ya kupunguza uzito hauna manufaa ya muda mrefu katika kupunguza mafuta mwilini miongoni mwa watoto na watu wazima.

Sukari hizo zisizo halisia na ambazo zinatumika ni pamoja na aspartame, advantame, cyclamates, neotame, saccharin, sucralose na stevia.

Kitu kibaya zaidi ambacho mapitio hayo yamebaini ni kwamba sukari hizo zisizo halisia zinaongeza hatari ya kupata uognjwa wa kisukari aina ya 2, magonjwa ya moyo na vifo miongoni mwa watu wazima.

Mkurugenzi wa WHO Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula Dkt. Francesco Branca amesema kuacha kutumia sukari ya kawaida na badala yake kutumia sukari zisizo halisia kwa muda mrefu hakusaidii kupunguza uzito.

Amesema “watu wanapaswa kufikiria njia mbadala za kupunguza matumizi ya sukari kwa kula vyakula vyenye sukari ya asili kama vile matunda au vinywaji na vyakula visivyo na sukari.”

Amesema “vikoleza utamu visivyo na sukari havina lishe yoyote. Watu wapunguze vyakula vitamu kwenye mlo wao tangu utotoni ili kuimarisha afya zao.”

WHO inasema pendekezo hilo linahusu watu wote isipokuwa wale wanaougua kisukari.

WHO imetoa onyo kwamba matumizi ya vikoleza utamu visivyo sukari hayapunguzi uzito | | Habari za UN Die WHO hat gewarnt, dass die Verwendung von zuckerfreien Süßungsmitteln nicht zu einer Gewichtsreduktion führt | UN-Nachrichten WHO has warned that the use of sugar-free sweeteners does not reduce weight | UN news La OMS advierte que el uso de edulcorantes sin azúcar no reduce el peso | noticias de la ONU L'OMS a averti que l'utilisation d'édulcorants sans sucre ne réduit pas le poids | Actualités de l'ONU WHOは無糖甘味料の使用は体重を減らさないと警告した|国連ニュース WHO ostrzega, że stosowanie słodzików bezcukrowych nie powoduje utraty wagi | Wiadomości ONZ A OMS alertou que o uso de adoçantes sem açúcar não reduz o peso | notícias da ONU 世卫组织警告称,使用无糖甜味剂并不能减轻体重|联合国新闻 世界卫生组织警告称,使用无糖甜味剂并不能减轻体重|联合国新闻

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, hii leo limetoa mwongozo unaoshauri watu wasitumie vikoleza utamu visivyo sukari halisia (NSS) kwa lengo la kupunguza uzito na kuepusha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs. The United Nations World Health Organization, WHO, today issued a guideline that advises people not to use natural sugar sweeteners (NSS) in order to lose weight and avoid non-communicable diseases, NCDs.

Assumpta Massoi anafafanua zaidi. Assumpta Massoi explains more.

Taarifa ya WHO iliyotolewa leo Geneva, Uswisi inasema mwongozo huo unafuatia mapitio ya ushahidi unaodokeza kwamba kutumia sukari isiyo halisia kwa ajili ya kupunguza uzito hauna manufaa ya muda mrefu katika kupunguza mafuta mwilini miongoni mwa watoto na watu wazima. A WHO statement released today in Geneva, Switzerland says the guidelines follow a review of evidence suggesting that using artificial sugar for weight loss has no long-term benefits in reducing body fat among children and adults.

Sukari hizo zisizo halisia na ambazo zinatumika ni pamoja na aspartame, advantame, cyclamates, neotame, saccharin, sucralose na stevia. The artificial sugars that are used include aspartame, advantame, cyclamates, neotame, saccharin, sucralose and stevia.

Kitu kibaya zaidi ambacho mapitio hayo yamebaini ni kwamba sukari hizo zisizo halisia zinaongeza hatari ya kupata uognjwa wa kisukari aina ya 2, magonjwa ya moyo na vifo miongoni mwa watu wazima. The worst thing the review found is that these artificial sugars increase the risk of type 2 diabetes, heart disease and death among adults.

Mkurugenzi wa WHO Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula Dkt. Director of the WHO Department of Nutrition and Food Safety Dr. Francesco Branca amesema kuacha kutumia sukari ya kawaida na badala yake kutumia sukari zisizo halisia kwa muda mrefu hakusaidii kupunguza uzito. Francesco Branca has said that giving up regular sugar and instead using artificial sugar for a long time does not help to lose weight.

Amesema “watu wanapaswa kufikiria njia mbadala za kupunguza matumizi ya sukari kwa kula vyakula vyenye sukari ya asili kama vile matunda au vinywaji na vyakula visivyo na sukari.” He said "people should think of alternative ways to reduce sugar consumption by eating foods with natural sugar such as fruits or drinks and foods without sugar."

Amesema “vikoleza utamu visivyo na sukari havina lishe yoyote. He said "sweeteners without sugar do not have any nutrition. Watu wapunguze vyakula vitamu kwenye mlo wao tangu utotoni ili kuimarisha afya zao.” People should reduce sweet foods in their diet from childhood to strengthen their health."

WHO inasema pendekezo hilo linahusu watu wote isipokuwa wale wanaougua kisukari. The WHO says the recommendation applies to all people except those suffering from diabetes.