×

Мы используем cookie-файлы, чтобы сделать работу LingQ лучше. Находясь на нашем сайте, вы соглашаетесь на наши правила обработки файлов «cookie».

Who is She?, 22- Unafanya Nini Hapa? – Текст для чтения

Who is She?, 22- Unafanya Nini Hapa?

Начинающий 1 Урок суахили для практики чтения

Начать изучать этот урок прямо сейчас

Nini kinaendelea hapa katika nyumba yangu?

Habari, Jina langu ni Naomi na huyu ni Anna.

Nafurahi kukutana nawe.

Unafanya nini katika nyumba yangu?

Mimi ni dadake Ibrahim.

Huyu ni Anna, rafiki yangu.

Sijali wewe ni nani.

Unafanya nini hapa?

Nani akufungulia?

Usikasirike.

Kwani, mimi ni dadake Ibrahim.

Hivyo mimi si mgeni.

Kwa nini Anna amevaa nguo la kulala na amelala kitandani?

Ninaweza kueleza.

Unajua Anna alikuwa amechoka na ...

Uliingiaje ndani ya nyumba yangu?

Mtu aliye chini aliniruhusu niingie, kwa sababu nilimwomba kufanya hivyo.

Yeye ni mtu mzuri.

Alikufungulia?

Ana haki gani kukuruhusu uingie hapa?

Tafadhali nieleze sababu ya rafiki yako kuwa kitandani changu na nguo za kulala, tena ni alasiri.

Nilishakueleza.

Amechoka na alitaka tu kulala kidogo kabla ya Ibrahim kuja nyumbani.

Learn languages from TV shows, movies, news, articles and more! Try LingQ for FREE